6/02/2022

Msichana ni Mzurii Lakini Haeleweki..Naombeni Ushauri

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA
Kuna msichana ambaye ni Jirani yangu sana na kusema kweli ni mzuri sana. Nilipataga hofu ya kumtongoza kwa sababu ya uzuri wake na ni gate kali. Ila kila alipokuwa anapata upenyo anakuja getto kwangu tunacheki movies na kula kwangu.

Siku moja nikajisemea moyoni kuwa Jamii na masela wangu wataniona kama sitampa mtoto haki yake mbali na kumuoa. Basi kidume nikajipanga na alivyo kuja kwa mara ingine gheto nikampa makavu live bila kupepesa macho. msichana aliniangalia na hakuweza kusema kitu akang'oa nanga na kuondoka.

Sikuwa na haja ya kumsihi arudi kwani alikasirika,ila moyoni nilijua massege sent. Ikapita kama wiki mbili bila kumwona tena ila kwa bahati nilikuwa nakatiza mtaani nikakutana nae akitokea sokoni nikampa hi na akaipokea bila kusita.

Nilivyompita na kumwacha nyuma aliniita "Ras" Lete habari,naomba unisaidie haka kamfuko huku akinitazama kwa jicho la madaha akiashiria kukubalian na ile sms nliyomtumia.

Basi tukiwatunasonga na safari huku story za hapa na pale nikaona ni vyema kumuuliza vp juu ya ile sms. Cha ajabu alikasirika zaidi ya mwanzon na kuninyang'anya kale ka mfuko na kuniambia nimemboa na hataki kampan yangu wala swaga zangu.

Naommbeni ushauri wenu nimfanyie Suprise gani huyu msichana ili anielewe kuwa nampenda.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

3 comments:

  1. Napenda sana story za mapenzi. Kwa kweli ulikuwa na aslimia kubwa sana ya kumpata ila uliaribu mwenyewe.Yaani uliwasha gari na kuondoka bila kuchemsha mafuta. Hukupaswa kumwambia kitu cocote kuhusu mapenzi, unge muiga kwanza ujue ni vitu gani anapenda na asivyo vipenda. Baadaye unakua unampa story nzuri hususani zile wewe unajua kwamba yeye hua anapenda, kisha unaanda chakula kinywaji ao vitu tu vya kutafuna wakati mna tizama filamu, na kinywaji pia kisikose. Hapo baasi usimuoneshe eti unamtetemekea hapana mshike tu kama ni wakawaida ila unamjali na hapo naamini matokeo yange likua mazuri baadaye.

    ReplyDelete
  2. branza madem ndo walivyo huyo manzi hawezi kukupa jibuj moja kwa moja vuta subira tu na mambo yatakua mwake

    ReplyDelete
  3. kuna madem hata usubiri miaka mia hawata lala na wewe. ni bora ungeendelea na urafiki tu sasa umetibua kimoja

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger