google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mtandoa wa TikTok uko mbioni kuondoa VIDEO ya mtu aliyekuwa akijitoa uhai | UDAKU SPECIAL

Mtandoa wa TikTok uko mbioni kuondoa VIDEO ya mtu aliyekuwa akijitoa uhai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Matandao wa kijamii wa TikTok unajitahidi kuondoa kanda ya video inayomuonesha mtu akijjitoa uhai. Video hiyo ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mtandao huo kwa siku kadhaa, ilianzia kwenye Facebook na sasa imeanzakusambazwa Twitter na Instagram.


TikTok ni maarufu kwa vijana wadogo – na baadhi yao wameripotiwa kutazama video hiyo na wamepata usumbufu wa kimwazo.

Mtandao huo umesema utawapiga marufuku akaunti za watu watakaoendelea kusambaza video hiyo mara kadhaa.

”Tunawashukuru wafuatiliaji wa mtandao wetu ambao wameripoti kuhusu video hiyo na kuwatahadharisha wengine dhidi ya kuitazama ama kushirikisha maudhui kama hayo kwenye jukwaa lolote, kwa heshima ya mtu huyo na familia yake” mwakilishi wa TikTok alisema.

Kwa upande wake Facebook imeiambia BBC: “Tulifuta video hiyo mwezi uliopita kwenye mtandao Facebook, siku iliyooneshwa moja kwa moja, na kutumia mfumowa teknolojia kufuta nakala za video zinazochapishwa kutoka wakati.

“Tunatoa pole zetu kwa familia ya Ronnie na marafiki wakati huu mgumu.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad