9/14/2020

Muna Love 'Naenda Msikitini, Sipangiwi Imani'MTUMISHI wa Mungu na masanii, Muna Love, ameeleza kuwa hawezi kupangiwa kwenye imani na kuna wakati anaenda hadi msikitini kwa sababu mama yake alikuwa Muislam.

Amesema ameamua kuishi kwenye maisha yake binafsi, hataki kupangiwa kitu chochote kwenye upande wa kumtangaza Mungu kwani Waislam na Wakristo wote sawa na nia yake ni kufikisha ujumbe.

“Sasa hivi naishi maisha yangu binafsi na maisha ya mtandao, pia nina mapatano yangu na Mungu ambayo hakuna mtu anayejua nitafanya kitu ambacho sijali binaadam atasema nini, najua simkosei Mungu.

“Mimi nipo kwa ajili ya kumtangaza, kuna wakati naenda hadi msikitini kwa sababu hata mama yangu alikuwa Muislam,. kwa hiyo siwezi kupangiwa kwenye imani, naamini wote tupo sawa,” ameeleza Muna Love.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger