9/10/2020

Museveni: Sihitaji kulumbana na vijana mitandaoni ili kuwashawishi, wengine wananiambia mimi mjingaRais wa Uganda Yoweri Museveni, amekuwa akizungumzia mkakati anaotumia kuwavutia vijana katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na wale ambao “wananitukana ,wakisema, wewe ni mjinga sana”.

Alisema mkakati wake ni kufanya mijadala thabiti ili kuwashawishi wakosoaji wake.

“Sihitaji kulumbana na hawa watoto ili kuwashawishi, nikituma ujumbe kuwajibu kumi waliokuwa wakinishambulia, sita pekee wanabakia na wane wananijibu wakisema mzee ametoa hojanzuri.”

Bwana Museveni ameongoza Uganda tangu 1986 na atagombea urais kwa muhula wa sita katika uchaguzi mkuu ujao.

Miongoni mwa wale wanapanga kumpinga katika kinyang’anyiro hicho ni msanii aliyegeuka mwanasiasa Bobi Wine, 38, wambaye ni maarufu kwa vijana.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger