9/24/2020

Mwanaharakati maarufu wa kutetea demokrasia HongKong akamatwaMwanaharakati maarufu wa Hong Kong anayepigania demokrasia, Joshua Wong amekamatwa. Hayo ni kwa mujibu wa ujumbe uliochapishwa kwenye ukurasa wake wa Twita. Wong alikamatwa baada ya kuripoti katika kituo kikuu cha polisi cha mji huo wa Hong Kong leo Alhamisi. 

Ujumbe ulioandikwa katika ukurasa wake wa Twita umeeleza kwamba kukamatwa kwake kunahusiana na kushiriki katika mkusanyiko uliopigwa marufuku mnamo mwezi Oktoba mwaka jana. 


Mwanaharakati huyo ameambiwa kwamba amekiuka sheria ya kupinga kujifunika nyuso kwa mujibu wa ujumbe wake. 


Tukio hilo limehusishwa na marufuku iliyotolewa dhidi ya kujifunika nyuso katika maandamano ambayo ilipitishwa na upande mmoja kinyume na katiba na mahakama ya rufaa ya Hong Kong mwaka jana. 


Mji huo wa Hong Kong ulikumbwa na maandamano makubwa ya umma mnamo mwezi Juni mwaka jana ya kupinga muswaada wa wahalifu wa Hong Kong kupelekwa China, muswada ambao hivi sasa umefutwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger