9/01/2020

Mwanamuziki Toni Braxton Ajutia Kuchelewa Kuanza Kufanya Mapenzi


Unamshauri nini Toni Braxton ambaye amesema kwamba anajutia kwa kutofanya sana mapenzi kipindi cha ujana wake?

Toni Braxton ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 52 na yupo kwenye mahusiano na Birdman, amesema kukulia kwenye mazingira ya dini kumemfanya achelewe kuanza masuala ya mapenzi na hata kunywa pombe, hivyo anatamani kipindi hiki ndicho angekuwa ametulia na kufurahia maisha

"Ninajuta kwa kutofanya sana mapenzi kipindi nilipokuwa kijana. Nilipaswa kunywa sana pia. Nilipaswa kujirusha sana pia, na hata kuvuta sana. Nafikiri kukulia kwangu kwenye dini kumenizuia kufanya mambo mengi ambayo nilipaswa kufanya. Sio picha nzuri kwa umri nilionao sasa, Kwa jinsi ilivyo inatakiwa ufanye haya mambo kwenye miaka 20 hadi 30 kisha ukifika kwenye 40 unatakiwa kutulia." amesema Toni kwenye gazeti la The Guardian.

Mwimbaji huyo na mwana televisheni, aliolewa mwaka 2001 na Keri Lewis na kufanikiwa kupata watoto wawili. Waliachana kwa talaka mwaka 2013. Mwezi Mei Mwaka 2016 alianza mahusiano na Birdman, Februari 2018 walitangaza kuvishana pete ya uchumba.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger