google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mwili wa mama mzazi P Funk Majani kuzikwa Uholanzi | UDAKU SPECIAL

Mwili wa mama mzazi P Funk Majani kuzikwa Uholanzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwili wa mama mzazi wa mtayrishaji wa muziki wa BongoFleva P Funk Majani, Aunt Sheilah umeshindikana kurudi ili kuzikwa Tanzania kwa sababu ya changamoto ya usafiri na Ugonjwa wa Corona, hivyo unatarajiwa kuzikwa leo nchini Uholanzi.


Mwenyekiti wa kamati wa maandalizi wa msiba huo ambaye ni msanii Soggydogg Anter, amesema mwili utazikwa Uholanzi na P Funk mwenyewe yupo huko kwa ajili ya mazishi, ambapo atarejea Tanzania Ijumaa usiku na siku ya Jumamosi watafanya dua maalum kwa marehemu.


“Siku ya leo tunatarajia mwili wa mama mzazi wa P Funk Majani Aunt Sheilah kuzikwa nchini Uholanzi, imebidi azikwe huko kwa sababu usafiri ulikuwa mgumu na wenzetu bado wana wasiwasi na ugonjwa wa Corona, P Funk Majani mwenyewe tayari yupo huko kwa ajili ya mazishi na atarejea Tanzania siku ya Ijumaa usiku, kisha Jumamosi itafanyika dua ya marehemu nyumbani kwake Bamaga mahali ambapo ipo studio za Bongo Records” amesema Soggydoggy Anter


Mama wa P Funk Majani alifariki nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu siku ya Septemba 8, na taarifa kuhusu kifo chake zilitoka Tanzania siku ya Septemba 10.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad