Nahodha Yanga Huyu Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



YANGA itaondoka kesho Septemba 25, 2020 jijini Dar es Salam kuifuata Mtibwa Sugar, lakini ishu ya nani atakuwa nahodha mpya kwa sasa bado imekuwa siri, huku majina yaliyopendekezwa na kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic yakipelekwa kwa mabosi ili kuthibitishwa, ila kuna nyota watano wenye nafasi ya kuwarithi Papy Kabamba Tshishimbi na msaidizi wake, Juma Abdul.


Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Zlatko alisema ameshapata akili ya nani atakuwa nahodha wa timu hiyo katika kipindi cha wiki tatu alichokaa na wachezaji wake, lakini akagoma kutaja kwa sasa akisema ni mpaka viongozi watakapoyapitisha.



 

“Nimekaa hapa wiki tatu sasa hilo suala la nani anakuwa nahodha nimeshapata akili ya nani namuona lakini bado nataka kwanza niongee na viongozi niwasikie nao wana mawazo gani,” alisema Zlatko.


“Unajua hii ni timu na ina utaratibu wake na inawezekana hata utamaduni wake naweza kuona huyu ni mtu sahihi, ila kumbe kule kwa viongozi nikawapa wakati mgumu, sitaki hilo litokee.”


Alisema anataka awe na nahodha atakayekubalika kwake, wachezaji wenzake na hata viongozi ambapo muhimu kwake aweze kuwaongoza kwa mfano wenzake wakiwa uwanjani.


MMOJA NDIYE


Licha ya Kocha Zlatko kutotaja majina, lakini kwa wiki tatu akiwa na timu amekuwa akiwatumia viungo Deus Kaseke na Haruna Niyonzima na beki Lamine Moro kama manahodha, lakini mmoja wapo kwa mujibu wa vigezo vya kupewa unahodha anaweza kuwa ndiye.


Mmoja ya viongozi wa Yanga alilidokeza Mwanaspoti kati ya wachezaji hao anaweza kuwa ndiye Nahodha Mkuu na akapatikana pia msaidizi wake.


Hata hivyo, Kocha wa zamani wa Yanga, Kennedy Mwaisabula ‘Mzazi’ alisema ili mtu awe nahodha wa timu ni lazima awe na sifa zifuatavyo, kuwa kiongozi na kusikilizwa na wenzake mwenye kuunganisha wachezaji na viongozi na kuchuja anachokiwasilisha, usupa staa ndani ya timu, kupata nafasi ya kucheza kikosini mbali na kuitumikia timu kwa muda mrefu na kujua miiko na tamaduni zake.


“Ni lazima mchezaji awe na sifa hizo, ndio maana mara nyingi manahodha wanakuwa na mastaa wa timu, yaani wenye ushawishi na kusikilizwa, pia mwenye nafasi kikosini, kwangu ningetakiwa kuteua mmoja, basi Niyonzima angefaa zaidi, ila Kocha Zlatko ndiye mwenye uamuzi wa mwisho,” alisema Mwaisabula.


Kwa vigezo vya sifa hizo, alizozianisha Mwaisabula, Lamine Moro, anaonekana kuwa anakidhi kwa namna yake ya ushawishi uwanjani akielekeza wenzake, pamoja na kiungo raia wa DRC, Mukoko Tonombe.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad