9/26/2020

"Natumaini CHADEMA wataniunga mkono"- KubeneaMgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia ACT Wazalendo,  Saed Kubenea, amesema kuwa hata kama vyama vya upinzani vitaamua kuungana na kuachiana baadhi ya majimbo ya uchaguzi, anayo imani kuwa chama cha CHADEMA kitamuunga mkono na kuhakikisha anapata ushindi katika jimbo hiloKauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 26, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa licha ya kwamba amechelewa kuzindua rasmi kampeni zake kutokana na matatizo yanayomkabili, lakini kampeni zake atazindua rasmi siku ya kesho ya Septemba 27,
"Mimi ni mtiifu wa maelekezo na maamuzi ya chama changu na kama chama kitasema jimbo la Kinondoni anaachiwa CHADEMA basi mimi nitakubali kuachia hilo jimbo ili mgombea wa CHADEMA aweze kugombea, lakini mimi matumaini yangu kwa kuwa mgombea wa CHADEMA anaweza kupata Ubunge kupitia dirisha lingine la viti maalum, naamini CHADEMA wataniunga mkono mimi ili hatimaye Kinondoni iweze kuongozwa na mimi", amesema Kubenea.
Aidha kubenea ameeleza ni kwa namna gani kesi yake mahakamani imemrudisha nyuma, "Matatizo yamenirudisha nyuma sababu yamevuruga mipango niliyokuwa nayo, yamenifanya niwe 'busy' na kesi badala ya kufikiria uchaguzi, nimepoteza mawasiliano sababu simu yangu ipo polisi, lakini pia yameniimarisha sana na nipo imara bado".

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger