Nedy Music "Situmii Kiki Kukuza Mziki Wangu"


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nedy Music amjibu shabiki yake katika ukurasa wake wa Instagram kuwa hatumii kiki ili kuendeleza muziki wake


Nedy music alimjibu shabiki huyo kwa kumwambia hatumii kiki kama wasanii wengine ili kukuza muziki wake.


"Broh I don't do kiki,nafanya muziki ambao watu wamenijua kupitia huo na kunisapoti." Nedy music aliandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Pia mashabiki wamemuuliza kuhusu kutoa kazi zake mpya maana amekaa kipindi kirefu bila kutoa nyimbo ambapo imepelekea mashabiki zake kukosa burudani ya muziki kutoka kwake 


Nedy music amewaahidi mashabiki hao kuwa hivi karibuni atatoa ngoma mpya ambayo itawafanya mashabiki zake waburudike tena

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments