NHIF Yakanusha Taarifa Juu Ya Kusitisha Utoaji Huduma Baadhi Ya Dawa.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Na Faustine Gimu
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)umekanusha taarifa zinazoenea kwenye Mitando ya kijamii kuwa umesitisha utoaji wa baadhi ya dawa kwa watumiaji wahuduma hiyo

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma Sept 5,2020  katika ofisi za Mfuko huo Mkurugenzi Mkuu Benard kongaamesema taarifa hizo  zimeleta taharuki kwa wanachama wake

Amesema mfuko huo umejenga imani kubwa kwa wateja wake tangu kuasisiwa kwake mwaka 2001 kwa sasa una dawa 543 ambazo zikinyambulishwa zinafanya idadi ya  dawa 975  baada ya kuongeza kitita cha mafao mwaka 2016

Amewatoa hofu wanachama wa NHIF hapa nchini  na kuwataka kuendelea kutumia huduma hiyo na kutoa rai kwa wananchi kuepuka kutoa taarifa ambazo si sahihi.

Sept 4 mwaka huu zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini(NHIF)umezifuta dawa 138 kutoka orodha ya dawa zinazotolewa na mfuko huo kwa wanachama wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad