Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

“Nilivuliwa Nguo Nikabaki Mtupu Makaburini” - Maye

 


Mtangazaji wa kipindi cha Dadaz ya East Africa TV Maye Kidoti amesema amewahi kujihusisha na masuala ya kishirikina na kufikia hatua hadi ya kwenda kwa mganga ili mradi awe maarufu lakini ikashindikana.

 

Akizungumza hayo wakati wanajadili mada ya kipi kinasababisha watu kwenda kwa waganga Maye Kidoti amesema yeye amewahi kwenda kwa mganga na akafuata masharti ya kubaki mtupu makaburini lakini bado hajafanikiwa.


"Nilishawahi kwenda kwa waganga na nishavuliwa nguo nikabaki mtupu huku mganga alikuwa ananiona na kunizungusha kwenye kaburi ambalo nilikuwa sijui la nani, kilichonipeleka kwa mganga ulikuwa ni ujinga wa kutafuta umaarufu na sikuupata mpaka nilipoachana na hayo mambo na kuamua kuokoka" amesema Maye Kidoti


"Pia nilishaenda kwa waganga wa vitabu na bado wakanipa nazi kuvunja njia panda, hii hali ya kupewa nazi kupeleka njia panda ni sawa na uchawi tu kwa sababu unajikuta unamshirikisha Mungu mambo ya waganga sio sawa, asikwambie mtu waganga ni waganga tu hakuna wa kutibu wala wa tunguli" ameongeza 

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments