9/06/2020

Ninja: Kwa Yanga Hii, Wasubiri Makombe Tu



BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema kutokana na ubora wa kikosi cha wachezaji walichonacho anapata uhakika wa kubeba makombe katika msimu ujao, Ligi Kuu Bara pamoja na michuano mingine watakayoshiriki.

Ninja ambaye ameanza kucheza sambamba na beki mpya wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto ametoa kauli hiyo kufuatia kuwa na muunganiko mzuri kwa wachezaji wa kikosi hicho.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ninja alisema kuwa, umefi ka wakati kwa mashabiki wa timu hiyo kuanza kupata furaha ya makombe kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kwani uongozi wa timu hiyo umefanya mabadiliko makubwa ya kiufundi.

“Ukweli naona tumekuwa na timu nzuri ambayo italeta ushindani na jambo kubwa kwetu wachezaji ni kuweza kujituma ili kufi kia malengo na nitacheza na mchezaji yeyote ambaye nitapangwa naye kwa sababu tunataka kufi kia malengo ya pamoja.

“Ndoto kubwa kwa mashabiki ni kupata ya makombe ndiyo jambo ambalo kwao wamekuwa na kiu nalo katika kipindi kirefu, binafsi naamini kwa timu ambayo tupo nayo basi wajiandae kuyapokea makombe japo tunatambua ushindani wa ligi utakuwa mkubwa lakini kwa umoja wetu tutafanikiwa,” alisema Ninja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger