Nukuu za Tundu Lissu "Wagombea Hawaenguliwi Wanapashwa Kusaidiwa na Tume Kujaza Fomu'

 


"Haijawahi kutokea tangu tumeanza Chaguzi Nchi hii wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa uwingi kama mwaka huu, naiomba Tume ya Uchaguzi (NEC) iwarudishe haraka iwezekanavyo wagombea wetu wote walioenguliwa”-Lissu akiwa Tabora

“Tume ya Uchaguzi isimamie Uchaguzi wenye wagombea wa CCM na wa Vyama vingine, kuengua Watu namna hii hakujengi Nchi kutabomoa Nchi, kama Tume haitowarudisha wagombea tutaungana na ACT Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nchi nzima" -LISSU

"Malawi ni ka-Nchi kadogo Wagombea hawaenguliwi, wanasaidiwa na Tume kujaza fomu, pale ambapo Mtu haelewi Msimamizi anamsaidia kujaza fomu, hakuna anayeenguliwa Malawi,Kenya na Nchi nyingine zenye Demokrasia, Tume iwarudishe walioenguliwa" -LISSU

"Maendeleo ya vitu siyo maendeleo ya binadamu, pamoja na kwamaba watu wanahitaji vitu kwa ajili ya maendeleo yao" - @TunduALissu

.

"Kama kuwa na Ndege nyingi ni maendeleo, basi Ethiopia ingekuwa ya kwanza kwa sababu ina Shirika kubwa la Ndege  kuliko nchi nyingine yoyote Afrika nzima" - @TunduALissu 

Mgombea Urais kupitia @ChademaTz

.

"Waethiopia wanakimbia nchi yao kwa maelfu, wanakimbia nini kama kuna hayo maendeleo?, wanakimbia kwasababu gani? wanakimbia kwa sababu hakuna uhuru, wanakimbia kwa sababu hakuna haki,kwa sababu hakuna demokrasia" @TunduALissu Mgombea Urais kupitia @ChademaTz

.

"Kwenye kitabu chake Baba wa Taifa anasema hivi, maendeleo maana yake ni maendeleo ya watu, barabara, majengo, ongezeko la uzalishaji mazao na mambo mengine ya aina hii hayo sio maendeleo ni vitu tu vinavyowezesha maendeleo" - @TunduALissu

.

"Sisi tunasema hivi ili tusitoze kodi ya kujifungulia na kodi ya oparesheni, nitahakikisha kwamba kila Mtanzania na kila mkazi wa Tanzania anapata Bima ya Afya" - @TunduALissu

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments