9/25/2020

Panya wa Tanzania mwenye uwezo wa kubaini mabomu apata nishani ya dhahabu UingerezaPanya mkubwa kutoka Afrika amepewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini.

Magawa ameweza kunusa mabomu 39 na silaha 28 ambazo hazijalipuka katika maisha yake.


Shirika la matibabu ya wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA limemtuza medali ya dhahabu “kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia”.


Inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu milioni sita ya kutegwa ardhini katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia. Nishani ya dhahabu ya PDSA, imeandikwa maneno “Kwa juhudi za wanyama au kujitolea kazini “.


Kwa wanyama 30 waliopewa tuzo hiyo, huyu ni panya wa kwanza.


Panya huyo aliye na miaka saba alipewa mafunzo na shirika lisilo la kiserikali- Apopo kutoka Ubelgiji lenye makao yake nchini Tanzania.


Shirika hilo limekuwa likiwalea wanyama wanaofahamika kama – Panya Shujaa- kugundua uwepo wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu miaka ya 1990.


Wanyama hao wanafuzu baada ya kuwapa mafundisho.


“Ni heshima kubwa kwetu kupokea tuzo hii,” Afisa Mkuu Mtendaji wa Apopo, Christophe Cox aliambia shirika la habari la Press Association. “Lakini pia ni ushindi mkubwa kwa watu wa Cambodia, na watu wengine duniani ambao wamekuwa wakiteseka kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini.”


Siku ya Ijumaa PDSA itatangaza mubashara hafla ya kumkabidhi Magawa tuzo hiyo katika tovuti yake.


Kulingana na Apopo, Magawa – aliyezaliwa na kulelewa Tanzania – akiwa na uzani wa kilo 1.2 (2.6lb) na urefu wa senti mita 70 (28in) .


Japo ni mkubwa kuliko spishi zingine za panya, Magawa ni mdogo ni mwepesi kiasi kwamba hawezi kulipua mabomu akitembea juu.


Panya hao wanafundishwa kubaini kemikali iliyotumiwa katika vilipuzi, kumaanisha wanaweza kupuuza vyma vikuukuu na kutafuta mabomu kwa haraka zaidi. Wanapopata kilipuzi wanakuna juu yake na kuwaonesha binadamu wafanyakazi wenzao.


Magawa ana uwezo wa kusaka mabomu katika eneo lenye ukubwa wa uwanja wa mpira wa tennis kwa muda wa dakika 20 – jambo ambalo Apopo linasema itamchukua mtu aliye na kifaa cha kubaini vifaa vya chuma kati ya siku moja hadi nne.


Panya huyo anafanya kazi kwa saa moja na nusu kwa siku nyakati za asubuhi na anakaribia kustaafu, lakini mkurugenzi mkuu wa PDSA Jan McLoughlin amesema kazi yake katika shirika la Apopo ilikuwa “ya kipekee na ya kuridhisha”.


“Kazi ya Magawa inaokoa na kubadilisha maisha ya binadamu ambao wanaathiriwa na mabomu hayo ya kutegwa ardhini,” aliambia shirika la hapari la Press Association. “Kila uvumbuzi anaopata unapunguza hatari ya kujeruhiwa au kufariki kwa watu.”


Kwa mujibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la kuondoa mabomu- HALO Trust, Cambodia imerekodi zaidi ya watu 64,000 waliojeruhuwa na wengine 25,000 kukatwa viungo vya mwili kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini kutoka mwaka 1979. Wengine walifariki wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo miaka ya 1970 na 1980.


Mnamo Januari 2020, Rais wa Marekani Donald Trump aliondoa vikwazo vya matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini kutoka Marekani ambavyo vilikuwa vimewekwa na Rais Barack Obama mwaka 2014.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger