Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Petitman: Inaniuma Kuitwa Mbeba Pochi wa Wema Sepetu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMENEJA na mjasiriamali Petitman Wakuache amefunguka kuwa alikuwa anaumizwa na maneno ya watu mitandaoni kiasi cha kufikia hatua ya kuchanganyikwa kwa watu kumuita mbeba pochi wa ‘Madam’ Wema Sepetu.


 


Amesema urafiki wake na Wema Sepetu umedumu kwa miaka 15, hivyo kwa sasa hata watu wakimtukana watakuwa wanajisumbua bure kwani hakuna tusi jipya.


 


“Zamani nikitukanwa mitandaoni ilikuwa inaniuma sana hadi nachanganyikiwa siku nzima kuanzia kuitwa mbeba pochi wa Madam Wema Sepetu lakini sasa hivi hata siumii kwa sababu hakuna tusi jipya,” amesema.


 


Aidha ameongeza kusema; “Madam Wema Sepetu anapambana sana, inaweza kupita hata wiki mbili bila ya kuonana kwa sababu anarekodi filamu yake, urafiki wetu unaenda mwaka wa 15 sasa, upande wa mwili wake sioni kama ni tatizo ikiwa yeye mwenyewe anaufurahia na kuupenda.”

Post a Comment

0 Comments