9/28/2020

Polepole aelezea na kusikitishwa na kifo cha Mwenyekiti UVCCM mkoa wa IringaKatibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole aelezea yaliyomsibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa, marehemu Emmanuel Polycupy Mlelwa hadi kukutwa na mauti huku akilitaka jeshi la polisi kuendelea kufuatilia tukio hilo.


Akiwa kwenye mkutano wake na waandishi  leo Septemba 27, Polepole amesema kuwa  Chama cha Mapinduzi kimefuatilia jambo hilo kwa uchungu mkubwa.


“Tunafahamu, sitaki kusema ili nisiingilie upelelezi wa polisi wamefanya mawasiliano na huyu kijana, wameomba kukutana naye, wakamteka, wamepotea naye tumekuja kukuta mwili wa kijana huyu eneo la Kibwena bwawani, amepigwa ameumizwa, amepoteza maisha yake” alisema Polepole


Aidha Polepole ametoa rai kwa jeshi la polisi  kufanya upelelezi huku akisema  kuwa hawako tayari kufanya siasa kwenye nchi hii inayomwaga damu.


“Sisi CCM tumefuatilia natunatoa rai kwa jeshi la polisi tafadhali wakati mwingine upelelezi unachukua muda bila sababu ya msingi, kipindi hiki ukweli unajulikana hatuko tayari kufanya siasa katika nchi hii tunamwaga damu nakupoteza maisha ya watanzania akiwemo kijana huyu mdogo” alisema Polepole.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger