Polisi Uganda kupima DNA za familia inayodai mtoto aliyekatwa kichwa ni wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Manaume aliyekamatwa na kichwa alisema alitaka kuwasilisha mzigo kwa Spika Rebecca KadagaImage caption: Manaume aliyekamatwa na kichwa alisema alitaka kuwasilisha mzigo kwa Spika Rebecca Kadaga

Polisi nchini Uganda wametibitisha kuwa kichwa cha mtoto kilichokatwa, kilichopatikana katika kikapu cha mwanaume aliyekamatwa kwenye lango la bunge nchini Uganda Jumatatu,kilikuwa ni sehemu ya mwili uliopatikana katika wilaya ya masaka, kusini- magharibi mwa mji mkuu Kampala


Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai nchini humo anasema wachunguzi watafanya kipimo cha vinasaba DNA kwa wajumbe wa familia moja ya Masaka ambao waliripoti kupotea kwa mtoto wao, kubaini iwapo kweli mtoto huyo aliyekatwa kichwa ni wao.


Familia iliyompoteza mtoto iliviambia vyombo vya habari nchini humo Jumanne, kwamba walikuwa wamemuajiri Joseph Nuwashaba, mwenye umri wa miaka 22, ambaye alipatikana na kichwacha mtoto, kama mfanyakazi wa shamba leo.


Uchunguzi bado unaendelea kubaini ni yapi yalikuwa malengo ya Bwana Nuwashaba, na polisi wamesema watafanya uchunguzi juu wa akili yake.


Alipokamatwa Bwana Nuwashaba aliwaambia maafisa katika bunge kwamba alitaka kuwasilisha mzigo uliokuwa na kichwa kwa Spika wa Bunge Bi Rebecca Kadaga.


Spika hajatoa kauli yoyote juu yatukio hilo, na aliwaambia wabunge kuwa anasubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad