Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Polisi Vietnam washikilia maelfu ya kondom zilizotumika

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREPolisi nchini Vietnam wamezishikilia zaidi ya kondomu 320,000 zilizotumika, ambazo ziliuzwa tena kinyume na sheria kwa wateja ambao hawakuwa na wasiwasi juu ya bidhaa hizo, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Video inayoonesha mkusanyiko wa mikoba mingi ikiwa na uzito wa kilogramu 360 katika ghala ambalo lilivamiwa hivi karibuni kusini mwa mji wa Binh Duong.


Mwanamke mmoja ambaye aliaminika kuwa mmiliki wa ghala hilo alikamatwa.


Kondomu ziliripotiwa kuwa zilikuwa zinaoshwa na kunyooshwa kwa maumbile ya bandia na kuweka tena kwenye makasha kabla ya kuuzwa tena.


Mwanamke aliyekamatwa alisema alikuwa analipa chini ya nusu dola $0.17 (£0.13) kwa kilo moja ya mfuko uliojazwa kondomu, kwa mujibu wa chombo cha habari cha taifacha Vietnam-VTV.


Haijawekwa wazi bado ni kondomu ngapi ambazo tayari ziliuzwa tena sokoni na watu wangapi walishanunua.Post a Comment

0 Comments