google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Polisi ya Urusi inataka kumuuliza Navalny maswali nchini Ujerumani | UDAKU SPECIAL

Polisi ya Urusi inataka kumuuliza Navalny maswali nchini Ujerumani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Polisi ya Urusi imesema leo kuwa inapanga kumuhoji kiongozi wa upinzani Alexei Navalny mjini Berlin, baada ya serikali ya Moscow kupuuzilia mbali kauli ya Ujerumani kuwa alipewa sumu inayoathiri mishipa ya fahamu ya Novichok.

 Polisi ya Urusi imesema kufuatia ripoti kuwa Navalny ameanza kupata fahamu, huenda watahitaji kumuuliza maswali ya ufafanuzi na ya ziada, na wawepo wakati wenzao wa Ujerumani wakiendelea na uchunguzi wao na Navalny, madaktari na watalaamu. 


Serikali ya Urusi inapinga majaribio yoyote ya kuilaumu Urusi kwa tukio hilo la sumu, na inasema inataka kujua nini kilitokea. 


Wanasiasa wa kimataifa wanasema tukio hilo linalonekana kuamrishwa na serikali na kuitaka Urusi ithibitishe kutohusika kwake. 


Mkosoaji huyo wa serikali ya Urusi mwenye umri wa miaka 44 na mwanarakati wa kupambana na rushwa aliugua baada ya kupanda ndege katika mkoa wa Siberia na akalazwa huko kabla ya kusafirishwa Ujerumani.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad