9/12/2020

Poshy: Wanawake Wanaongoza Kwa ChukiMrembo ambaye alijizolea umaarufu hivi karibuni baada umbo lake kuonekana kuwavutia watu mbalimbali bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy’ amesema alichojifunza kwenye dunia hii, wanaoongoza kwa chuki na roho mbaya ni wanawake na sio wanaume.


Akizungumza na Amani, Poshy, alisema kuwa amegundua kuwa kuna wanawake wengine hawapendi kuona mwingine anaendelea hivyo mwanamke huyo akiona mwenzake anapiga hatua, atamuwekea kila aina ya chokochoko ili kumtibulia mambo yake.“Watu wanashindwa kuelewa kuwa huku duniani kila mtu ana bahati yake hivyo ukiona mwenzako anafanikiwa au mwanamke mwenzako anafanya vizuri mshike mkono uzidi kumfanya ainuke ili akuinue na wewe na sio kumponda kila kukicha maana huo utaitwa ni wivu,” alisema Poshy ambaye tayari amejikwamua kwa kufungua duka lake la kuuza nguo za ndani.

Stori: Imelda mtema
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger