google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html R Kelly Akutana na Kisanga Kingine Gerezani | UDAKU SPECIAL

R Kelly Akutana na Kisanga Kingine Gerezani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



STAA wa muziki wa kiwango cha Dunia kutoka nchini Marekani, Robert Kelly ‘R Kelly’, amekutana na kisanga cha kushambuliwa na mahabusu mwenzake gerezani, ambako anasubiri hukumu ya kesi yake.

Akizungumzia ishu hiyo, mwanasheria wa R Kelly, Steve Greenberg amesema, mteja wake huyo alishambuliwa katika gereza hilo la Chicago Metropolitan Collection Center, ambako R Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake ya unyanyasaji wa kingono wa wanawake.


Mahabusu mwenzake na R Kelly, alimshambulia alipokuwa amekaa kwenye kitanda kwa kumpiga ngumi sababu ikiwa kusitishwa kwa kutembelewa gerezani kutokana na mashabiki wa R Kelly wanaoandamana nje ya gereza hilo.


R Kelly amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na kushindwa kupewa dhamana ambapo kesi yake hiyo, inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Septemba.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad