9/03/2020

Rais Magufuli amuahidi kazi aliekuwa Mbunge Shinyanga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameahidi kumtafutia kazi ingine aliekuwa Mbunge wa Shinyanga Stephen Masele ambaye nafasi yake ya kuwania Jimbo hilo imechukuliwa na Katambi ambaye alikuwa DC Dodoma.
“Yale mengine ya pembeni achaneni nayo, Katambi ni kijana nampenda mpeni kura, atawavusha, jana tu nimekutana na Masele aliyekuwa Mbunge wa hapa wala sina tatizo, mimi ni Rais nitamtafutia kazi nyingine, ukishakuwa Rais Makazi yapo mengi tu”-JPM

“Masele nitamtafutia tu kazi ya kwenda kufanya, ukishakuwa Rais kazi ni nyingi, hata leo kuna nafasi ya Mtu mmoja anafanya hovyohovyo huko, Katambi ameacha Ukuu wa Wilaya Dodoma Makao Makuu kuja kuomba kura Shinyanga anawapenda, Katambi ukichaguliwa usibadilike kama wengine”-JPM
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger