Rihanna Amefunguka Mapya Kuhusu Mahusiano yake na Chris Brown.


Wakati wengi wakidhani kwamba uhusiano wao ulikufa mwaka 2009 mara baada ya Breezy kumpa kipigo mrembo huyo, Kwenye mahojiano na Oprah Winfrey kupitia Podcast yake "Supersoul Conversation" Riri amesema bado wanapendana sana na daima wataendelea kuwa marafiki wa karibu

"Tumeendelea na urafiki wetu tena, kwa sasa sisi ni marafiki wa karibu sana. Tumerudisha uaminifu tena na kwa hivyo tunapendana sana tutafanya hivyo kila siku. Na hicho sio kitu ambacho kitaenda kubadilika, hicho sio kitu ambacho unaweza kukizima au kukiepuka, kama ulishawahi kuwa kwenye mapenzi." amesema Rihanna.

Rihanna hakuishia hapo, aliendelea kwa kusema "Nafikiri alikuwa mpenzi wa maisha yangu. Alikuwa mpenzi wangu wa kwanza. Na ninaona ananipenda kama mimi ninavyo mpenda, wala sio kwamba eti tutakuwa pamoja. Ninampenda sana. Kitu kikubwa kwangu ni kwamba ana amani. Mimi sitakuwa na amani kama yeye atakuwa hana furaha hata kidogo, au akibaki mpweke." alikazia Riri.

Kwa maneno hayo ya Rihanna, unaona penzi la wawili hawa likirejea? Tuachie comment yako

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments