9/24/2020

Rosa Ree Ashirikishwa na Christian Bella Kwenye Wimbo Utakao Zinduliwa Tarehe 02 OctoberMKALI wa muziki wa dansi Christian Bella asema bado yeye ni mkali hata akikaa kimya miaka 100 bado ni Msanii anaekubalika kutokana na upekee wa sauti yake .


Bella amekiri kuwa toka mwaka huu uanze haja achia ngoma kwa sababu ya maandalizi ya ujio wa albam yake mpya ambayo ameipa jina lake CBO.


"Niwatoe hofu mashabiki zangu kuwa albam yangu mpya imekamilika na nitaanza kuachia nyimbo moja kila wiki,"


Ambapo Bella amesema leo 23 septemba ataachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la "Pacha" 


"Pacha ni moja wapo ya wimbo ambao upo katika albam yangu ambayo imebeba vibao 11 na video," 


Aidha, ameongeza kuwa ndani ya albam hiyo upo wimbo ambao amemshirikisha mwanadada Rosa lee anaefanya vizuri katika mziki wa HIPOP nchini.


"ngoma niliyomshirikisha Rose Lee inaitwa "Only you" hii natarajia kuizindua kwenye onyesho maalum October 2 katika club ya The Base jijini Dar es salaam.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger