9/26/2020

Sababu ya Whozu kufuta picha zake zote Instagram

 


Msanii wa BongoFleva Whozu amefunguka sababu za kufuta picha zake zote katika ukurasa wake wa Instagram kutokana na kutambua mabadiliko aliyonayo kwa sasa

 

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Whozu amesema aligundua hakuwa na sababu ya kuwa na picha hizo.


“Ukurasa wangu ulikuwa mchafu sana ilikuwa na vitu ambavyo sio vitu vya kazi baada ya kufikiria nikaona nifute kwa sababu safari ya muziki bado inaendelea, namuomba Mungu aendelee kuniweka hai hayo ni maamuzi tu ya mtu ,yoyote anaweza vitu nilivyofuta havikuwa na muelekeo niliamua tu kufuta” amesema Whozu


Kwa upande mwingine Whozu amefunguka kuhusu muonekano na mitupio yake kwa kusema "Suala la kupendeza linatokana na kuishi katika fashion, nimezaliwa kwenye familia inayopenda mitindo, watu wanaonizunguka wamechangia kuwa katika mazingira hayo, kingine nina duka la nguo kwa hiyo ni baraka tu hizo".


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger