Saed Kubenea apandishwa kizimbani, Akosa dhamana na Kurudishwa rumande

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Jimbo la Ubungo aliyemaliza muda wake Saed Kubenea amepandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arusha akituhumiwa kwa makosa mawili likiwemo la kutatisha fedha na kuziingiza nchini bila kibali.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Martha Mahumbuga jopo la mawakili wanne wa serikali wameeleza kuwa mnamo tarehe tano mwezi wa tisa huko Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya mtuhumiwa alikutwa na dola za Kimarekani 8000 hela za Kenya 491,700 na  fedha za Kitanzania 71,000.

Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kukiuka sheria za kuvuka mpaka kwenda nchi jirani ya Kenya na kurejea nchini Tanzania kwa kutumia  njia zisizo rasmi.

Kutokana na kosa la kutakatisha fedha kutokuwa na dhamana mtuhumiwa amepelekwa gerezani hadi tarehe 21/09/2020 kesi hiyo  itakapotajwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad