Samatta Afunguka Kwa Mara ya Kwanza "Siondoki Aston Villa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ataendelea kukipiga katika klabu ya Aston Villa  inayoshiriki Ligi Kuu England.

Aston Villa imenusurika  kushuka daraja msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya 17  katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 35.

Timu hiyo ilifanikiwa kubaki baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham inayofundishwa na kocha David Moyes.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Samatta alisema anajivunia kubaki Ligi Kuu England kwa msimu mwingine.

“Nataka kumshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine tena, napenda kuwashukuru mashabiki waliokuwa nyuma yangu, kuiombea Villa kubaki msimu ujao, nawaomba waendelee kuomba ili na mimi niendelee kubaki hapa,” alisema Samatta.


Samatta alijiunga na  klabu ya Aston Villa  akitokea Genk ya Ubelgiji  kwa kitita cha pauni milioni 8.5 (zaidi ya sh bil. 25 za Tanzania).


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad