Sarpong, Tonombe Wampa Jeuri Niyonzima Yanga SC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




KIUNGO mchezeshaji fundi, raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima, ametamba kuwa wana kila sababu ya kuuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na usajili bora mpya uliofanywa na timu hiyo.


Kauli hiyo aliitoa wakati timu hiyo ikiwa kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa ligi uliotarajiwa kupigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Tanzania Prisons.

Wachezaji baadhi waliosajiliwa na Yanga ni Michael Saprong, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Faridi Mussa, Yacouba Songne, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior na Kibwana Shomari.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema kuwa kati ya vitu ambavyo wamevifanya uongozi wa timu hiyo ni usajili ulio bora wenye wachezaji wa viwango tofauti na msimu uliopita.

Niyonzima alisema kuwa usajili huo bora utaongeza hali ya ushindani wa namba katika timu kutokana na kila mmoja kuwepo kwenye kiwango kizuri katika kuhakikisha wanapata matokeo.

Aliongeza kuwa katika msimu uliopita, timu yao ilikuwa na upungufu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo anaamini ndiyo ilisababaisha waukose ubingwa wa ligi.

“Msimu huu lazima uwe wetu Yanga, hiyo ni kutokana na usajili bora uliofanyika hasa katika safu ya ushambuliaji ambayo ndiyo ilisababisha tuukose ubingwa.“Kama safu ya ushambuliaji ingekuwa bora, basi tungechukua ubingwa msimu uliopita, kwani washambuliaji wetu walikuwa wanapata nafasi nyingi za kufunga ambazo walishindwa kuzitumia.


“Lakini ujio wa washambuliaji wapya utaiwezesha timu kupata matokeo mazuri ya ushindi, kikubwa viungo tunatakiwa kutengeneza na kutumia nafasi zote tunazozipata kuhakikisha tunazitumia vema kwa kufunga mabao,” alisema Niyonzima.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad