9/01/2020

Saudia yamfuta kazi kamanda wa kijeshi kwa madai ya rushwaMfalme Salman wa Saudi Arabia amewafuta kazi watu wawili wa familia ya Kifalme na akawaweka chini ya uchunguzi wa ufisadi katika wizara ya ulinzi pamoja na maafisa wengine wanne wa kijeshi. 


Amri hiyo ya Mfalme Salman imesema Mwanamfalme Fahd bin Turki Abdulaziz Al Saudi ataondolewa kwenye wadhifa wake wa kamanda wa majeshi ya pamoja katika muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita nchini Yemen, na mtoto wake wa kiume Mwanamfalme Abdulaziz bin Fahd ameondolewa kwenye nafasi yake ya naibu gavana wa jimbo la al-Jouf.


 Uamuzi huo umetokana na barua ya Mrithi wa kiti cha Ufalme Mohammed bin Salman kwa kamati ya kupambana na ufisadi ya kuitaka ichunguze shughuli za kifedha zinazotiliwa shaka katika wizara ya ulinzi. 


Mwanamfalme Salman amelipa kipau mbele suala la vita dhidi ya rushwa katika mageuzi anayoyafanya nchini humo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger