Senzo Awatuliza Yanga SC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Senzo Awatuliza Yanga SC



MMOJA wa mabosi wa Yanga, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini, amefunguka kwa kuwafuta hofu mashabiki wa timu hiyo akiwaambia watulie kwani kikosi hicho kitakuwa hatari kadiri muda unavyooenda.


 


Senzo ameongeza kwamba kwa sasa mashabiki wa timu hiyo watulie kwani kikosi ndiyo kinazidi kujijenga kwa ajili ya kufanya makubwa kwenye Ligi Kuu Bara na michuano mingine msimu huu.




Yanga katika usajili wa msimu huu, imesajili wachezaji 12 katika kukiimarisha kikosi hicho kinacholisaka taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa tatu mfululizo bila ya mafanikio.


Senzo ameliambia Spoti Xtra kuwa, kikosi hicho kwa sasa kinaendelea kujijenga taratibu ambapo mashabiki wake wanatakiwa watulie kwani watakuja kupata kitu ambacho wanakitaka wakikaa sawa.

“Japo tumepata pointi kwenye mechi zote mbili lakini bado mashabiki wanatakiwa kutulia kwa sababu kikosi bado kinaendelea kujijenga taratibu.

“Benchi la ufundi linafanya kazi hiyo na tunaamini baada ya muda kila kitu kitakaa sawa, ila watupe muda kwa kipindi hiki, wasubirie baada ya muda mambo yakikaa sawa watapata kile ambacho wanakitaka,” alimaliza Senzo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad