9/26/2020

Sijawaogopa Sadio Mane, Mo Salah itakuwa Kagere na Chama, Papaa Zahera atuma salam Simba

 


Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Gwambina ya jijini Mwanza, Mwinyi Zahera amesema mechi yao dhidi Simba chochote kinaweza kikatokea kwakuwa Simba ni timu kubwa nchini lakini kikosi chake kipo tayari kukabiliana nao siku ya Jumamosi Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar Es Salaam.

 

Akiongea na Kipenga , East Africa Radio, Zahera amesema pamoja na ubora wa kikosi cha Simba pamoja na kuwa na wachezaji wenye viwango vikubwa nchini lakini kamwe hawezi kutishika na ukubwa huo.


“Mimi nimeshacheza na Sadio Mane, Mohamed Salah lakini sikuwaogopa vipi nije kuwaogopa kina Kagere na Chama ingawa ni wachezaji wazuri, nawaheshimu lakini siwezi kuwaogopa” amesema Zahera.


Aidha, Kocha huyo amesema ili waone ukubwa wa Simba basi wawafunge zaidi ya goli nane kwakuwa hata Barcelona waliwahi kufungwa goli nane na Buyern Munich ya Ujerumani katika nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya mwezi Agosti 2020


Itakumbukwa Kocha Mwinyi Zahera aliwahi kuifundisha Klabu kongwe nchini Yanga msimu wa 2018-19 na katika msimu wa 2019-20 alifungashiwa virago kikosini humo kutokana na kuwa na muendelezo mbovu wa matokeo katika msimu wake wa mwisho.


Gwambina bado haijapata ushindi katika michezo mitatu iliyopita ambayo walipata suluhu dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kufungwa na Ruvu Shooting na Biashara ya Mara huku ikiwa haijafunga goli hata moja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger