9/06/2020

Simba Waanza Ligi vizuri, Dodoma nao Wabishi


Mechi 5 kati ya 6 za ufunguzi wa msimu wa ligi kuu soka Tanzania bara 2020-21, leo Septemba 6, 2020 zimemalizika.


Magoli ya John Bocco na Mzamiru Yassin yamewapa ushindi mabingwa watetezi Simba SC huku wageni wa ligi kuu Dodoma Jiji FC ambao wamepanda daraja wakipata ushindi wa kwanza.

Katika timu tatu zilizopanda ligi kuu msimu huu, mbili zimepoteza mechi zake.

Gwambina wakiwa ugenini dhidi ya Biashara United wamefungwa goli 1-0, huku Ihefu nao wakifungwa na Simba 2-1 wakiwa nyumbani.

Matokeo yote

Ihefu FC 1-2 Simba SC
Dodoma Jiji 1-0 Mwadui FC
Mtibwa Sugar 0-0 Ruvu Shooting
Namungo 1-0 Coastal
Biashara 1-0 Gwambina
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger