Sitaki kuona Moo Dewji anakorofishwa - Tunda Man

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Msanii na shabiki wa Klabu ya Simba Captain Tunda Man amesema hataki kumuona mwekezaji wa Klabu hiyo Mohammed Dewji "Moo Dewji" anakorofishwa au anakerwa na kwa kitu chochote ndani ya Klabu hiyo.

Tunda Man amesema Moo Dewji ameipa heshima Simba ambapo awali walikuwa wanadharaulika pia amefanya vitu vikubwa na malipo yake hapaswi watu kumkera ili asiweze kuisaidia tena Simba.


Tunda Man amefunguka kuwa, "Kila mtu ana mapungufu yake hata kama binadam anakosea,  kilichotokea sikitafsiri vibaya, sitaki kuongea sana ila Moo Dewji amefanya mambo makubwa ndani ya Simba, pia sitaki kuona Moo anakorofishwa kwa kitu chochote na vitu vikubwa ambavyo amevifanya hivyo malipo yake yasifanywe kwa kitu ambacho kinaweza kumkera" 


Tunda Man amesema hivyo kufuatia siku kadhaa zilizopita kuibuka hoja kwenye mtandao wa Twitter kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla akihoji mustakabali wa Bilioni 20 ambazo mwekezaji wa Klabu ya Simba Moo Dewji aliahidi atazitoa.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad