9/21/2020

Snura "Mwanamke wa Kwanza Kuvalishwa kofia na Rais, Mungu Akitaka Kukuheshimisha Hakuna Anaeweza Kukudharaulisha"

 


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye pia ni mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi CCM leo septemba 21, 2020 ameendelea na utaratibu wake wa kuwavalisha kofia wasanii ambapo leo Menja Kunta na Snura ndio waliobahatika kuvalishwa kofia hizo.

Baada ya tukio hilo Snura Mushi amejigamba na kuwa yeye amekuwa mwanamke wa kwanza kuvalishwa kofia na Mh. Rais.


Kupitia ukurasa wake wa instagramu ameandika haya;


''Nashukuru sana kuwa MWANAMKE WA KWANZA KUVISHWA KOFIA NA RAISI WETU JPM..

MSANII WA KIKE WA KWANZA RAIS KUVUA KOFIA YAKE NA KUNIVALISHA (hii ni kubwa sana kwangu).. Ndani ya mkoa wa TABORA sitosahau historia hii, kwangu Mimi ni baraka kubwa sana nimepewa leo na Mh Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuniheshimisha NAKUSHUKURU SANA NA ASANTE SANA, ama kwa hakika huyu ni Raisi mwenye upendo sana, na kupitia chama changu cha MAPINDUZI leo nimepata heshima hii kubwa kama mwanamke.. Asanteni sana viongozi wangu wote wa chama๐Ÿ™๐Ÿ™..

"HAKIKA Mungu akitaka kukuheshimisha hakuna anaeweza kukudharaulisha ALHAMDULILLAH MUNGU UMENIJIBU JIBU KUBWA SANA.

CCM OYEEE ๐Ÿ’š๐Ÿ’š MAGUFULI OYEEE'' @snuramushi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger