Sven Aongezewa Majembe Matano Kuiua Mtibwa


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mechi zote za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na ile inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki dhidi ya Yanga inayotarajiwa kuchezwa Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa.Tayari Simba imeshamalizana na Ihefu, Septemba 6 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine na ilikosa huduma ya majembe yake matano ambao walikuwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Gerson Fraga aliyekuwa na matatizo ya kifamilia, Ibrahim Ame aliyekuwa akisumbuliwa na majeraha ,Chris Mugalu, Luis Miqussone na Pascal Wawa ambao hawakuwa na utimamu wa mwili ‘match fi tness’.Akizungumza na Championi Jumatano, Ofi sa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa wachezaji wote wapo fi ti na wanaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Septemba 12, pamoja na mechi nyingine.“Tunajiandaa vizuri kwa ajili ya mechi zetu zote ikiwa ni pamoja na ile ya wenzetu, sasa taarifa niliyopewa ni kwamba tayari Gerson Fraga yupo Bongo, Ame ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha naye yupo vizuri na mchezo wetu wa kwanza wachezaji wetu hawajaumia hilo ni jambo zuri.“Malengo yetu ili yatimie ni lazima tupate matokeo kwenye mechi zetu zote, tunatambua kwamba ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa lakini tupo tayari, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema.Simba inakutana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri ambapo msimu uliopita mchezo wa mwisho walipokutana uwanjani hapo, Mtibwa Sugar ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0, hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wa kisasi.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments