9/21/2020

Swizz Beatz, Alicia Keys Wampa Kazi MondiMTAYARISHAJI  nyota wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz, amejitokeza na kueleza juu ya alichofanya mwanamuziki maarufu wa Tanzania, Diamond Platnumz, kwenye album ya saba ya Alicia Keys iitwayo  ALICIA.

Mkali huyo Kasseem ‘Beatz’ Dean anaeleza Diamond awaeleweshe mashabiki kuwa kwenye wimbo ambao ameshirikishwa alifanya kulingana na maamuzi yake, jambo ambalo baadhi ya mashabiki walionyesha kuwa Diamond amewapa kiasi kidogo cha burudani.

Diamond anasikika akitumia lugha ya Kiswahili katika uandishi wake kwenye wimbo  wa ‘Wasted Energy’ kutoka kwenye album hiyo ambapo aliimba kwa sekunde zisizozidi ‘30’ mwisho wa wimbo.

Ikumbukwe Album ya ALICIA itakuwa  ya 13 kutoka kwa Alicia Keys na album ya kwanza ndani ya miaka mitatu tangu alivyoachia album yake ya mwisho iitwayo Dirty Dancing 2 mwaka 2017.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger