9/22/2020

Tajiri Mkosoaji wa Rais Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 18 Jela ChinaKorti moja nchini China imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 18 jela kwa tajiri mmiliki wa majengo Ren Zhiqiang, ambaye ni mkosoaji wa rais wa nchi hiyo, Xi Jinping. 

Korti hiyo ya mjini Beijing imemkuta tajiri huyo na hatia ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma. Ren mwenye umri wa miaka 69 alikuwa mwanachama wa chama tawala cha kikomunisti, na mwenyekiti wa kampuni ya Huayuan Properties, na alikuwa na urafiki na maafisa waandamizi wa chama hicho, akiwemo makamu wa rais Wang Qishan. 


Mapema mwaka huu, tajiri huyo na mwanawe walitoweka kwa muda, baada ya kutunga shairi lililokosoa namna serikali ya rais Xi Jinping ilivyolishughulikia janga la virusi vya corona. 


Alifukuzwa kutoka chama tawala mwezi Julai, akituhumiwa kula njama na watoto wake za kujirundikia mali bila kikomo. Korti hiyo imesema Ren Zhiqiang amekiri makosa yake na kuomba msamaha.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger