google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html TAKUKURU Hanang yaondoa milango 83 iliyowekwa kwenye Kituo cha Afya Chini ya Kiwango | UDAKU SPECIAL

TAKUKURU Hanang yaondoa milango 83 iliyowekwa kwenye Kituo cha Afya Chini ya Kiwango

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Hanang mkoa wa Manyara imemuamuru Mzabuni Ayubu Iyaka  aliyepewa kazi ya kutengeneza na kupachika milango kwenye jengo la kituo cha Afya cha Hirbadaw, kuondoa milango yote 83 aliyoweka kwenye kituo hicho baada ya kubainika haina Ubora.


Takukuru imebaini hayo baada ya maafisa wake kufanya ukaguzi kwenye kituo hicho ambapo aliingia mkataba na Halmashauri hiyo kutengeneza na kupachika milango 83 yenye ubora iliyotengenezwa kwa kutumia mbao ngumu kwa gharama ya shilingi Milioni 28,000,000.


Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu  Septemba 24,2020, amesema wamejiridhisha kuwa kwa makusudi Mzabuni huyo aliamua kukiuka mkataba akatengeneza na kuweka kwenye jengo hilo la Kituo cha Afya milango hiyo isiyokuwa na ubora.


Pamoja na hayo  amesema Halmashauri ilishamlipa shilingi Milioni 14,000,000 ambazo ni nusu ya  fedha walizoingia mkataba.


Makungu amesema milango hiyo ambayo inadaiwa kuwa ni mipya, imeonekana ikiwa  imepasuka,mingine imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika.


Amesema kufuatia hayo Takukuru wilayani Hanang,  imemuamuru Mzabuni huyo kuondoa milango yote 83 na kutengeneza mingine yenye ubora unaokubalika katika majengo ya serikali na kwa mujibu wa mkataba alioingia na Halmashauri, na kwamba ataruhusiwa kuweka milango hiyo baada ya kukaguliwa na kujiridhisha kama ubora wake umekidhi vigezo.


Takukuru imewaasa  Wazabuni wanaopenda kufanya kazi na serikali kuwa waadilifu na kuzingatia mikataba ya kazi, huku ikitoa rai kwa watumishi wa Umma waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya Umma kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa katika ubora unaokubalika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad