9/05/2020

TAKUKURU: Ubwabwa Kwenye Kampeni ni RushwaMkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amemuonya Hashim Rungwe ambaye ni mgombea Urais kupitia CHAUMMA kuwa kugawa chakula ‘ubwabwa’ wakati wa kampeni ni rushwa na ni kosa kisheria.

Myava alisema Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inapiga marufuku kwa mgombea kutoa vitu kama chakula kushawishi wapigakura ili wamchague. Rungwe amekuwa akiwaalika wafuasi wajae kwenye kampeni zake ikiwemo uzinduzi utakaofanyika Manzese, Dar es Salaam leo Septemba 5 kwa kuahidi ubwabwa utakuwepo.


Myava amesema kipindi hiki kinachotakiwa ni kunadi sera ili kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua na si kushawishi kwa kutoa rushwa.


Rungwe amesema atatumia ubwabwa kama CCM wanavyotumia wasanii, amesema kufanya hivyo si rushwa na amewataka wajiandae kupelekana mahakamani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger