9/25/2020

Tetesi za Soka KimataifaManchester United wiki ijayo itaweka mezani dau la mwisho la £90m kwa ajili ya kujaribu kumsajili winga wa England Jadon Sancho, 20, kutoka Borussia Dortmund. (Mirror)

Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Chelsea na Italia Jorginho, 28. (Sky Sports - via Mail)


Lucas Torreira anakaribia kuondoka Arsenal, huku klabu za Atletico Madrid na Torino zikionyesha nia ya kumnasa kiungo huyo wa Uruguay, 24. (Independent)


Atletico Madrid wanaamini watamnasa Torreira kwa mkopo, hatua itakayoifanya Arsenal nayo kumsajili kiungo wa timu hiyo ya Hispania Thomas Partey, 27, raia wa Ghana. (Sky Sports)


Alex Telles anaamini kiwango cha fedha kilichotajwa na Porto kwa Manchester United kiasi cha £18.3m sio halisi kwa sababu mlinzi huyo wa kushoto wa Brazil, 27, atakuwa mchezaji huru msimu ujao. (Guardian)


Manchester City imesema madai kwamba imeweka ofa ya £78m kwa ajili ya mlinzi wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25, sio kweli. (Goal)


Monaco imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Tottenham na England Dele Alli, 24, (90min)


Paris St-Germain wanatarajia kujiondoa kwenye mazungumzo ya kumsajili Alli kwa mkopo wa muda mrefu. (Telegraph - subscription required)


Kiungo mchezeshaji wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 28, anaweza kwenda kwa mkopo Arsenal kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Star)


RB Leipzig wanakaribia kumsajili mlinzi wa kati, hatua itakayosaidia mlinzi wake Dayot Upamecano kuondoka klabuni hapo. Manchester United imekuwa ikihusishwa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21. (Star)


Mshambuliaji wa Napoli Arkadiusz Milik amewekwa sokoni kwa kikosi cha Everton cha Meneja Carlo Ancelotti, lakini Muitaliano huyo akiwa na joto la kutaka kuungana nae tena nyota huyo wa kimataifa wa Poland, 26. (Corriere della Sera - via Inside Futbol)


Sheffield United inaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Liverpool , Muingereza Rhian Brewster, 20, huku klabu za Aston Villa, Brighton na Crystal Palace zikionyesha nia ya kumsajili. (Independent)


West Ham na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka kumsajili kiungo wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 24, kwa mkopo wa msimu mzima. (Guardian)


Southampton wanatarajia pia kukamilisha usajili wa kiungo wa Toulouse na Ivory Coast Ibrahim Sangare, 22. (Telegraph - subscription required)


Everton na Fulham wanamuania mlinzi wa Cameroon Jerome Onguene, 23, kutoka RB Salzburg. (Sportslens)


West Brom wanaweza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester City Emmanuel Adebayor, 36, kama watashindwa kumnasa mshambuliaji mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Sun)


Mlinzi wa St Etienne Wesley Fofana anaweza kutua Leicester City lakini mpango wowote utakaokubaliwa utakaomfanya kinda huyo wa umri wa miaka 19 asalie kwenye Klabu hiyo ya Ufaransa. (L'Equipe - via Leicester Mercury)


Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl anataka kusajili wachezaji watatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Echo)


Bayern Munich hawatamruhusu kiungo wa Ufaransa Michael Cuisance kuondoka kwa mkopo, licha ya Leeds United na Marseille kuripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa umri wa miaka 21. (Sport Bild - in German)HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger