9/25/2020

Tuambizane tu ukweli ili tupate kilicho bora katika mahusiano ya kimapenziKwenye swala zima la mahusiano ya mapenzi pesa haina chochote cha kuthibitisha. Na anayetanguliza pesa mbele katika mapenzi hana upendo wala mapenzi ya kweli. 


Wanawake 

Usikimbilie kumpima imani mpenzi wako kwa kumuomba pesa ili ujue kama anakupenda au laa mwanaume ni kiumbe anayeweza kufanya kila unachotaka akamilishe malengo yake. 

Be careful utachezewa na utatumika sana lakini kumpata wa kuishi naye forever hutapata. 


Wanaume 

Kumpatia pesa mpenzi wako kila akihitaji hakumfanyi yeye akuone ni kiasi gani unampenda ila huenda ukageuzwa kitega uchumi chake. Lugha ya mjini tunaita atm yake. 


Unampomuapproach mwanamke epuka kumuonyesha maisha ambayo siyo level zako maana kama utampa pesa sana kabla ya kumuoa jiandae kufanya hivyo baada ya ndoa 

Ukishindwa black brother huna ndoa tena, Wahenga wanasema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" 


Nyote 

Epuka kuweka mbele katika mahusiano vitu ambayo vinaisha na kupotea kabisa kama pesa, mali na mengine mengi maana yakiisha hayo yatatengeneza hatima ya mapenzi yenu.. 


Busara yangu/ ushauri 

Katika mapenzi siku zote tanguliza moyo wako na hisia za kweli kwa uliye naye , mpe moyo wako na yeye akupe wake ila mambo mengine mungu atawapatia mbele kwa mbele. 


Kama nilichosema haifai na kimekuudhi utanisamehe lakini nimeongea ukweli na mambo ambayo yemetawala sana kwenye mahusiano ya sasa hivi. 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger