9/03/2020

Tundu Lissu "Sisi Hatuwezi Kuishi Bila Dunia"


Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameahidi kuwa atahakikisha anarudisha mahusiano mema baina ya Tanzania na Dunia nzima.

Lissu amesema hayo leo Septemba 2, 2020, akiwa anaendelea na uzinduzi wa kampeni kwa chama hicho kwa Mkoa wa Shinyanga, ambapo amesema nchi ya Tanzania haiwezi kuishi bila ya Dunia.

“Katika mambo ya kwanza ambayo tutayafanyia kazi ni kurudisha mahusiano mema na Dunia, sisi hatuwezi kuishi bila Dunia,Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia", alisema Tundu Lissu.

Aidha Lissu amesema kuwa ili kukuza uchumi wa nchi atahakikisha anajenga na kudumisha mahusiano mema na ulimwengu wote, "Serikali yetu katika kukuza uchumi wa nchi, lazima tujenge mahusiano mema na Dunia, hatuwezi kuishi bila Dunia, Dunia inaweza ikaishi bila sisi".
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger