9/25/2020

Tuwe wa Kweli....Unamchagua Tundu Lissu Kwa Lipi Hasa?Na Mwamba wa Kaskazini


Mpaka leo tafiti mbalimbali zinampa Rais Dkt John Pombe Magufuli ushindi wa zaidi ya asilimia 85 katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.


Hii tutaijadili wakati wake lakini bado najiuliza hivi hizo asilimia 6 wakati mwingine 4.5 ambazo tafiti nyingi zinaonesha Lissu atapata bado najiuliza wachache hao watakaopiga kura hizo zitakuwa za nini hasa?


*Hapa naainisha mambo 10 yanayonishangaza  kwa Lissu na kuonesha hafai hata kupata hizo asilimia 6 za kura za mwaka huu:*


1. Akiwa Mbunge hawezi kukuonesha hata mtaro wa maji aliosaidia kuujenga jimboni;


2. Akiwa Mbunge alisifika kwa kuzuia wananchi kushiriki maendeleo;


3. Akiwa Mbunge hakuwahi kupitisha bajeti yoyote kwa maendeleo ya wananchi zaidi ya kuzikataa zote;


4. Mpaka sasa hajawahi kusoma chochote anachoahidi kutoka kwenye Ilani kwani haijachapishwa na haijulikani iko wapi zaidi ya kuweka toleo lenye makosa lukuki mtandaoni;


5. Hakuna mahali popote amesisitiza amani zaidi ya vurugu na kuhubiri malalamiko;


6. Wanaonekana kuamini katika mataifa ya nje kuja kuwasaidia kwa kufikiri na kutekeleza. Huyu wasomi wengi wanasema atarejesha ukoloni mamboleo kwa kasi; 


7. Anaponda kila kitu cha nchi wakiwemo Waasisi wa Taifa, Lissu mara kadhaa anamtusi Nyerere, ashamtusi Mzee Mwinyi, Mkapa na JK na Magufuli wote kawatusi. Hana heshima ni mropokaji ni chizi;


8. Anaponda kila maendeleo yaliyopo nchini ikiwemo barabara wanazopita, maji wanayokunywa, umeme wanaoutumia kila siku n.k


9. Ni mwongo, tapeli na mtu asiye makini: Kila anachosema kuhusu Serikali hajafanya utafiti anaishia kudanganya. Alidanganya kuhusu Uwanja wa Ndege wa Mpanda akaumbuliwa; Alidanganya kuhusu reli ya Mpanda akaumbuliwa na alidanganga kuhusu bajeti ya ndege na mradi wa umeme sasa kaoneshwa mpaka vifungu vya bajeti iliyopitishwa na Bunge. Kamo ila bado atadanganya tena.


10. Ni muumini wa ushoga. Na hakika siku alizokaa Ulaya na kulipiwa fedha nyingi akiwa hospitali msimamo wake kwenye masuala ya kitaifa, rasilimali na maadili umeyumba sana haijulikani nini kimemtokea mpaka kawa muumini wa ushoga hasa. Na kashaahidi kufuta sheria zote zinazozuia ushoga nchini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger