9/29/2020

Uganda 'kufanyia binadamu majaribio' ya chanjo ya Covid-19Uganda natarajiwa kuanza kufanyia binadamu majaribio ya chanjo ya Covid-19 mwezi Novemba, Ripoti ya gazeti la Daily Monitor imewanukuu maafisa wa Wizara ya Afya.

Chanjo hiyo imeandaliwa kupitia ushirikiano kati ya Taasisi ya utafiti ya Uganda na Chuo Kikuu cha Uingereza.


Mkuu wa Jopokazi linalohusika na majanga Monica Musenero, amenukuliwa akisema awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo hiyo itafanyiwa Waganda 10.


Awamu ya kwanza ikifanikiwa, awamu ya pili itajumuisha watu kati ya 100 hadi 200 ikifuatiwa na awamu ya mwisho itakayojumuisha watu kati ya 1,000 na 3,000,alisema.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger