Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Uingereza yapandisha ngazi ya kitisho cha COVID-19Uingereza imepandisha kiwango cha tahadhari juu ya kitisho cha maambukizi wa virusi vya corona kutoka ngazi ya tatu hadi ya nne, kutokana na kuongezeka kwa kasi ya maambukizi mapya. 

Ngazi ya nne maana yake ni kwamba hatari ya kuambukizwa virusi hivyo ni ya kiwango cha juu. Wataalamu wa afya nchini humo wameonya kuwa ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa, Uingereza itaanza kushuhudia ongezeko la vifo kutokana na ugonjwa wa COVID-19. 


Mganga mkuu wa serikali ya England Chris Whitty amesema ifikapo katikati mwa mwezi ujao wa Oktoba, huenda Uingereza itakuwa ikisajili maambukizi mapya 50,000 kila siku. 


Tayari Uingereza ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na COVID-19 barani Ulaya, ikiwa imewapoteza watu wake 42,000 kwa janga hilo. 


Waziri mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson ametangaza mkakati mpya wa kuzuia kasi ya kuenea zaidi kwa ugonjwa huo, zikiwemo kupunguza muda wa huduma za baa na mikahawa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments