9/24/2020

Ulaya yalaumiwa kwa Mateso ya Wahamiaji Libya

 


Shirika la kimataifa la utetezi wa haki za bindaadamu la Amnesty International limeutupia lawama Umoja wa Ulaya kwa ukiukwaji haki za wakimbizi na wahamaji Libya.

 


Ripoti hii mpya ya shirika hilo lenye maskani yake mjini London, Uingereza imeukosoa Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama wake, kwa kuinga mkono serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya (GNA) yenye makao yake mjini Tripoli na kitendo cha kuweka ulinzi katika eneo la pwani ya Libya kwa lengo la kuzuia wakimbizi na wahamiaji wasiingie Ulaya na hatimaye kuwarejesha Libya.


Kwa Mujibu wa ripoti hiyo mpa pia, mateso yameongezeka kutokana na masharti ya kukabiliana na janga la la virusi vya corona.


Shirika la Amnesty limesema wamekuwa wakipelekwa katika vituo vya kuwahifadhi ambako wanawekwa kizuizini kiholela na bila ya ukomo jambo ambalo shirika hilo linaeleza kuwa si la kiutu.


Kambi hizo awali zilitengwa kwa ajili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Libya, kati ya wanamgambo wanaopigana bega kwa bega na serikali inayotambulika kimatiafa ya Libya na wapiganaji watiifu kwa mbabe wa kivita wa huko mashariki mwa taifa hilo, Khalifa Haftar, imegeuka kuwa ya umauti na maumivu kwa wahamiaji.


Umoja wa Ulaya hajatoa msukumo wowote kwa serikali ya Libya wa kukemea mateso.


Shirika hilo imesema Umoja wa Ulaya haujatoa shinikizo lolotea kwa serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kuheshimi haki za wakimbizi na wahamiaji. Markus Beeko ambae ni katibu mkuu wa Amnesty International kwa Ujerumani amesema pamoja na kuwepo kwa ahadi za kurebisha hali hiyo kulikotolewa na serikali hiyo lakini hali uhalifu umeendelea bila ya kuwajibishwa yeyote.


Tangu kuondolewa madarakani na kuuwawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Libya, 2011, Muammer Gaddafi, taifa hilo lenye utajiri wa mafuta limeingia katika machafuko na katika miaka ya hivi karibuni limekuwa uwanja wa mapigano kwa makundi hasimu. Mataifa ya Ulaya yamekuwa katika majaribio ya kutafuta suluhisho la vurugu hizo, ambazo zimetoa nafasi kwa wanofanya biashara ya usafirishaji haramu wa watu.


Amnesty: Mateso na manyanyaso ni ya muda mrefu.


Kwa miaka kadhaa Umoja wa Mataifa na makundi ya utetezi wa haki za binaadamu yamekuwa yakirejea kuonya kwamba wahamiaji nchini Libya wapo katika hatari ya mateso, unyanyaswaji wa kijinsia na usafirishaji haramu wa watu.


Katika ripoti hii mpya Shirika la Amnesty International limewahoji watu 42, wakiwemo wakimbizi 32 na wahamiaji ambao wengi waliwekwa kizuzini bila ya kufikishwa katika mikono ya sheria.


Wote 32 walitekwa kwa shinikizo la kutakiwa kulipa kikombozi na waliteswa, kubakwa au kunyimwa chakula hadi familia zao ziwanusuru kwa kulipa fedha. Amnesty limesema kwa mwaka huu pekee zaidi ya wakimbizi 5,000 wameondoshwa kwa lazima Libya ambapo baadhi yao wamekwama katika mipaka ya Sudan na Chad bila ya chakula au maji.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger