Uongozi sio madegre, Lusinde ni Mchapakazi – JPM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Haya ni mambo matano aliyoyazungumza Mgombea Urais Dr. John Pombe Magufuli (CCM) baada ya kusimama Mlowa ambako Mgombea Ubunge wa CCM ni Livingstone Lusinde, Dr. Magufuli alisimama Mlowa wakati akiwa njiani kuelekea Iringa ambapo haya hapa chini ndiyo aliyoyaongea.

“Nileteeni wa CCM ambao ninao uwezo wa kuwatumbua mkinileta mwingne sina uwezo wa kumtumhua pesa zitaliwa na sina cha kumfanya, Mbunge wenu Lusinde ni mchapakazi, narudia Ubunge sio Madegree ni uwezo wa kujenga hoja”


“Nawapenda sana watani zangu Wagogo, naamini kabisa mtanipa kura, tena inawezekana Lusinde akanitafutia Kasichana kazuri ka Kigogo au mnasemaje Wagogo?, si mtanipa?, zege halilali, RC Dodoma mwagize Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma huu mwezi wa tisa ndani ya miezi miwili Barabara ya Mlowa kwenda Mvumi itangazwe tenda kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami ili Wagonjwa wanaougua hapa wawe wanapelekwa Mvumi, tunataka Jimbo hili ambalo lipo karibu na Makao Makuu ya Nchi tulibadilshe liwe lenye kunusanusa makao Makuu”


“Mvumi nina historia nayo nilikuwa na Kaka yangu alikuwa Daktari pale sasa hivi ni Marehemu kwahiyo Mvumi ninaifahamu nilishawahi kumleta Mzee mmoja kutoka Chato ambaye alinishauri Mimi kujiunga na siasa nilimleta pale Mvumi kufanyiwa upasuaji”


“Hata kuhamia Dodoma haikuwa rahisi tumekaa zaidi ya miaka 47 hilo halijawezekana ila sisi tumeweza, tunajenga uwanja wa Ndege mkubwa Msalato, Ndege zote za Kimataifa zitakuwa zinatua hapa, tumejenga Reli ya kisasa, Soko la kissa, Stendi ya kisasa, tunataka kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Agwe Muwaha..!! MLungu akutaze Jemedali
    wangu.

    Nene ni Wachekulu wadatu, To Uze, Mkupelaje mmonga. Milimo ilibaho..!!

    Magu, Baba kura zetu Wana Dodoma kwa
    Ujumla wetu ni kwako kipenzi chetu.
    tarehe 27 Oct. hatupigi matap tapu
    tutadamka alfajiri ile Sala Salaa
    kuwahi kukupigia kura yako na Mbuge na Diwani wa CCM.

    Inshallah Mwenyezi mungu atakulinda Daima na hawa wana Saccoz Wapotoshaji/ wachonganishi /Wafitinishaji / Vibaraka / Na Siajabu, inawezekana Mashho**a (Ulaya ule chao,! hawakuachi salama) Na Ni wakosa Sera. Isitoshe
    Dozi za Muda Mrefu zimewaathiri Upstairs Na Wamekuwa Waropokaji bila
    kujielewa na kujitathmini.

    Magu Baba,Wembe n Ule ule. Mitano tena

    ReplyDelete
  2. Agwe Mdogo wa kukaya,Muwaha..!! MLungu akutaze Jemedali wangu.

    Nene nina Wachekulu wadatu, To Uze, Mkupelaje mmonga. Milimo ilibaho..!!

    Magu, Baba kura zetu Wana Dodoma kwa
    Ujumla wetu ni kwako kipenzi chetu.
    tarehe 27 Oct. hatupigi matap tapu
    tutadamka alfajiri ile Sala Salaa
    kuwahi kukupigia kura yako na Mbuge na Diwani wa CCM.

    Inshallah Mwenyezi mungu atakulinda Daima na hawa wana Saccoz Wapotoshaji/ wachonganishi /Wafitinishaji / Vibaraka / Na Siajabu, inawezekana Mashho**a (Ulaya ule chao,! hawakuachi salama) Na Ni wakosa Sera.

    Isitoshe hizo Dozi za Muda Mrefu zimemuathiri Upstairs.

    Na Wamekuwa Waropokaji bila kujielewa wala wenye kujitathmini.

    Magu Baba,Wembe n Ule ule. Mitano tena

    ReplyDelete

Top Post Ad