"Urais Nitashinda Tena Kwa Kura nyingi"- Magufuli Aweka Wazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amewahakikishia wananchi wa Kibondo mkoani Kigoma kuwa katika uchaguzi mkuu ujao atashinda kwa kura nyingi kwani Watanzania wa maeneo yote wanamtaka yeye.

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 17, 2020, wakati akiendelea na mikutano yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali huku akisisitiza wananchi kumchagulia madiwani na wabunge kutoka chama hicho.

"Nitasikitika sana kama hamtanichagulia wabunge na madiwani wa CCM kwa sababbu mimi Urais nitashinda tu tena kwa kura nyingi sana na ninataka niwahakikishie kwa sababu watanzania maeneo yote wanamtaka Magufuli", amesema Dkt Magufuli.

Aidha Magufuli akatoa rai kwa wana CCM wale ambao hawakuchaguliwa kuwani nafasi katika uchaguzi mkuu ujao, "Naomba wana CCM wenzangu mliokosa nafasi msinunue, kuchaguliwa pia ni mipango ya Mungu, yule mbunge wa Busanda amegombea mara nne, miaka mitano iliyopita nikamteua kuwa DC mwaka huu ndiye anayegombea pale, hata mliogombea mwaka huu msikate tamaa".

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii, Hainaga Shaka wala Mjadala. Ila wasindikizaji ni wengi na baadhi yao ni wakosefu wa Adabu na Nidhamu.

    Tutakupa tena Kazi Indelee.

    ReplyDelete

Top Post Ad