9/11/2020

Urusi Yakerwa na Marekani kuhusí madai ya kuhusika kumpa sumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny Urusi imesema kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, kwamba afisa mkuu wa serikali ya Urusi alihusika katika kumpa sumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, haikubaliki.

Awali, Pompeo alisema inawezekana afisa mwandamizi wa serikali ya Urusi aliamuru Navalny apewe sumu aina ya Novichok, na kuongeza kuwa dunia nzima inajua kilichotokea. 


Msemaji wa rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake inayo maslahi katika kujua undani wa yaliyomfika Navalny, na kuitaka Ujerumani kutoa ushirikiano kwa kuipa Urusi matokeo ya vipimo vya Navalny. 


Mapema leo, Waziri Mkuu wa Italia, Giussepe Conte alinukuliwa akisema ameambiwa na Rais Putin kuwa uchunguzi utafanyika kubainisha ukweli kuhusu masaibu ya Alexei Navalny, lakini baadaye Urusi imekanusha hilo, ikisema yumkini Conte alielewa vibaya. 


Navalny aliugua ghafla wakati akifanya kampeni kuelekea uchaguzi we serikali za mitaa utakaofanyika Ijumaa na Jumapili nchini Urusi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger